Skip to main content

Posts

UWE KARIBU NASI KWA HABARI NA MATUKIO

WAHARIRI WASIMAMIENI WAANDISHI WAANDIKE HABARI KWA WELEDI

  IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA @@@@ WAHARIRI kisiwani Pemba wametakiwa kuwasimamia vyema waandishi wao kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi, ili habari zao zilete mafanikio katika jamii. Akizungumza na wahariri katika Ukumbi wa TAMWA Chake Chake Pemba, Afisa Mawasiliano kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA), Sophia Ngalapi alisema kuwa, waandishi wengi tayari wameshapewa mafunzo kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa kupitia mradi wa kupambana na Mabadiliko ya tabianchi (ZanAdapt), hivyo ni jukumu la wahariri kusimamia ili ziandikwe habari zenye ubora. Alisema kuwa, kupitia sauti za wanahabari, wanaamini kwamba zitaisaidia jamii hasa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya tabianchi ambayo huathiri sana maendeleo katika maeneo wanayoishi. "Mabadiliko ya hali ya hewa yanaleta athari mbali mbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, hivyo kupitia kalamu za waandishi wataibua changamoto na kupatiwa ufumbuzi unaofaa kwa maslahi yao na taifa kwa u...
Recent posts

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WANAWAKE WAMEJITOKEZA, VYAMA VIWATEUE.

                                                                                                      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WANAWAKE WAMEJITOKEZA, VYAMA VIWATEUE.TAREHE:                                                                                    27/07/2025.  Wadau wa masuala ya wanawake na uongozi wanaviomba vyama vya siasa kuhakikisha kuwa vinawateua wanawake waliokidhi vigezo, kugombea nafasi za uongozi ndani ya vyama vyao kwenye uchaguzi wa ushindani ndani ya nafasi za uwakilishi, ubunge na udiwani....

JAMII IMETAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO WENYE ULEMAVU ILI KUWAJENGEA UELEWA

IMEANDIKWA NA REHEMA MOHAMED PEMBA@@@@ JAMII inashauriwa kuwa karibu na watoto wenye ulemavu, ili kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo elimu.zuh Hayo yalizungumzwa na sheha wa shehia  ya Chambani wakati  alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao. Alisema kuwa, watoto wenye ulemavu wanahitaji zaidi uangalizi wa mama na baba na sio kumuachia mzazi mmoja peke yake au kumtelekeza kwa bibi.  Alisema, katika jamii kuna baadhi ya watu mara baada ya kupata mtoto ambae ana ulemavu, huamua kumtenga na kumuachia katika uangalizi wa mzazi mmoja hususani mama ili kuweza kukaa nae na baadhi ya wakati kushindwa kuwapatia hata huduma. Alieleza kuwa, si jambo la busara kabisa kwa watoto wenye ulemavu kuwaweka nyumbani bila ya kuwapatia elimu, kwani nao wanayo haki ya kupata elimu bora, kupatiwa matibabu pamoja na mahitaji mengine kama watoto wengine. Vile vile alisema kuwa, ni vyema jamii iondoshe itikadi mbaya ya kuwa mtoto mwenye ulemavu hawezi kufanya chochot...

MWENYE ULEMAVU WA VIUNGO AOMBA KUPATIWA KITI MWENDO

IMEANDIKWA NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ Mohamed Omar Mohamed mkaazi wa Machomane Chake Chake Pemba mwenye ulemavu wa miguu, ameiomba Serikali na jamii kwa ujumla kumsaidia kupata kiti cha magurudumu (wheelchair) kitakachomuwezesha kuendeleza shughuli zake za kijamii na kiuchumi kwa wepesi zaidi. Akizungumza na ZanzibarLeo hapo nyumbani kwake Machomane, Mohamed amesema kiti ambacho amekuwa akikitumia kwa sasa kina zaidi ya miaka mitano na kimechakaa vya kutosha kiasi cha kushindwa kutembelea kwa mwendo unaoridhisha. Amesema kiti alichonacho hivi sasa kimepoteza nguvu na kimekuwa kikiharibika mara kwa mara, hali inayosabisha kubaki muda mrefu bila ya kiti hicho kutokana na ughali wa matengenezo yake. Amesema mara nying kiti hicho huharibika betri ambayo imekuwa ikiuzwa kwa bei ya Tsh. 80,000, kiwango ambacho si rahisi kwake kukimudu kutokana kipato chake kidogo. "Najiona dhaifu mno.  Kiti mwendo ndio miguu yangu nilojaaliwa na Allah. Kutokana na hali ngumu ya kimaisha, nashindwa kununua ...

'WARATIBU WA UCHAGUZI PITIENI SHERIA, KANUNI KWA UMAKINI': JAJI MSTAAFU

NA MOZA SHAABAN, PEMBA WASHIRIKI wa mafunzo ya uratibu wa Uchaguzi kisiwani Pemba wametakiwa kuzipitia na kuzifuata vyema sheria, kanuni, taratibu  na miongozo ya uchaguzi ili kutekeleza ipasavyo majukumu yao. Wito huo umetolewa leo Julai 21, 2025 na  Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mbarouk Salim Mbarouk ambae pia ni mgeni rasmi katika mafunzo hayo yaliofanyika Wawi Chake  chake Pemba. Alisema ni vyema kwa waratibu hao kutumia muda wao kuzisoma na kuzifuata katiba, sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi ili kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao katika kipindi chote cha usimamizi wa uchaguzi Mkuu. Alieleza kua uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbali mbali za kisheria, zinazopaswa kufuatwa ili kuimarisha utendaji wa kazi hizo pamoja na kuimarisha amani nchi. "uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbali mbali za kisheria zinazopaswa kufuatwa ili kuimarisha utendaji wa kazi  na kujua na kuzifuata sheria hizo kutasaidia  kuimari...

WANAWAKE WAHIMIZWA KUVITUMIA VYOMBO VYA HABARI KUTANGAZA KAZI ZAO

  NA MWANDISHI MAALUM@@@@ MENEJA miradi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) Nairat Abdulla amewaomba wanawake kutumia vyombo vya habari kwa lengo la kutangaza kazi zao wanazozifanya. Akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wakulima viongozi kutoka shehia nne (4) za Unguja, juu ya umuhimu wa kutumia vyombo vya habari, yaliofanyika ofisi za TAMWA-ZNZ Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja, amesema wanawake wanajishughulisha na harakati mbalimbali zikiwemo za uzalishaji pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lakini bado sauti zao hazisikiki ipasavyo kupitia vyombo vya habari. Hivyo amewaomba wanawake hao kutumia vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii, kuelezea mafanikio na changamoto zinazowakabili katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili kufikisha ujumbe kwa wahusika na hatimae kupatiwa ufumbuzi. Akiwasilisha mada inayohusu vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano kutoka TAMWA ZNZ, Sofia Ngalapi amesema wanawake waku...

WANAWAKE DAR -ES SALAAM WAOMBA ELIMU ZAIDI KUHUSU HAKI

NA MWANDISHI MAALUM@@@@ WANAWAKE Jijini Dar es salaam wameomba elimu ya haki za binadamu na misingi  ya utawala bora izidi kutolewa kwenye mikusanyiko ya wanawake kwani wao mara nyingi wamekuwa wakikosa fursa ya kupata elimu hiyo hasa katika mikutano inayoandaliwa na viongozi wa Serikali kutokana na majukumu waliyo nayo. Rai hiyo imetolewa na wanawake waliotembelea banda la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.   ''Tumejifunza mengi leo kuhusu haki zetu kama wanawake, tunaomba elimu hii itufikie hadi kwenye vikundi vyetu vya kina mama, kwani mara nyingi tunashindwa kuifikia mikutano inayoandaliwa vijijini ama mitaani kutokana na shughuli nyingi za jamii majumbani, lakini elimu ya haki ikitukuta kwenye vyama vyetu huwa tunalazimika kwenda kwasababu huwa haviwahusu wanaume”. alisema mama mmoja aliyetembelea banda ya THBUB, viwanja vya sabasaba. Kwa upand...

MKAGUZI WA POLISI SHEHIA YA PANDANI, AWAASA VIJANA KUJITENGA NA JINAI

  NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ MSAIDIZI shehia ya Pandani wilaya ya Wete, Inspekta wa Polisi Khalfan Ali Ussi, amesema, ushirikishwaji wa jamii katika dhana ya ulinzi shirikishi, kutasaidia vijana kujitambua na kuishi kwa kuzingatia madili katika jamii.   Aliyasema hayo mara baada ya kukamilika kwa bonanza la michezo, lilifanyika katika uwanja wa mpira katika kambi ya ‘FFU’ Finya wilaya Wete.   Alisema vijana ndio wahanga wakubwa katika jamii kwenye matokeo mbali mbali ya uhalifu, hivyo wanapaswa kupewa elimu itakayowawezesha kujitambua na kuacha matendo yaliyokinyume na maadili ya jamii.   Alieleza kuwa, kundi hilo nalo ni muhimu mno katika jamii ya leo na kesho, hivyo lazimalitazamwe kwa jicho pan ana kukua wakiwa na maadili mema.   "Mabonanza kama haya yakiendelea kufanyika yatawasaidia wao, kuhamisha akili yao katika matendo ya kihalifu na kushiriki katika michezo, ambayo tija yake ni kubwa,’’alifafanua.   Aidha aliwasisitiza vij...

SHERIA MPYA YA HABARI ZANZIBAR BADO NI KIZUNGUZUNGU

NA SITI ALI, ZANZIBAR@@@@ “Sheria ni msingi wa haki amani na maendeleo kwa kila nchi “Hayo si maneno yangu bali yalikuwa ni  maneno ya Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizindua toleo jipya la juzuu za sheria mwezi  Aprili ,2025 jijini Dar es salaam. Anasema, bila ya sheria kuwa wazi uhakika wa ulinzi wa haki za raia unatoweka au unakuwa hauna uhakika na kusababisha uvunyifu wa amani.    Wandishi wa Habari Zanzibar wamekuwa wakidai sheria nzuri na rafiki ya habari bila ya mafanikio yoyote.Kutokana na kutumia sheria ya zamaani na iliyopitwa na wakati  iliyotungwa tokea miaka ya 1988 ambayo kwa sasa ni kikwazo kwa wandishi wa habari. Akizungumzia kuhusu sheria hiyo, mwandishi nguli wa habari visiwani Zanzibar, Salma Lusangi anasema ni muhimu kwa sasa sheria hiyo ibadilishwe ili iendane na wakati na kukidhi matakwa ya wakati husika. “Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukifanya uchechemuzi wa sheria mbili kuu yaani sheria ya Wakala wa...

KUKUU KANGANI WAASWA KUJIEPUSHA NA WIZI WA KARAFUU

    BAKAR KHAMIS, PEMBA@@@@ WANANCHI kisiwani Pemba, wameaswa kuacha tabia ya wizi wa zao la karafuu, kwani kufanya hivyo pia wanaweza kuingizwa kwenye vitendo vya ukatili na udhalilishaji. Hayo yameelezwa na Mkaguzi wa Polisi Inspekta Hamad Ali Faki, kwenye kikao cha kuimarisha maadili ndani ya jamii, wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya Kukuu Kangani wilaya ya Mkoani.   Alisema wapo baadhi wanajamii, wamekuwa na tabia ya kukwapua karafuu za wenzao wanapokuwa shambani, jambo ambalo linaweza kusababisha madhara zaidi, ikiwemo udhalilishaji.   Alieleza kuwa, zipo kesi kadhaa kila unapofika msimu wa uchumaji wa zao karafuu, hujitokeza zikiambatana na wizi wa karafuu.   "Ndugu zangu wanajamii, niwasihi sana kujiepusha na dhulma ya wizi wa karafuu, maana ndio chanzo cha udhalilishaji, ikiwemo watoto kupewa mimba, kulawitiwa na wengine kuhujumiwa kwa kipgo,"alifafanua.   Katika hatua nyingine, aliwakumbusha wazazi na walezi, kutowaac...